Ukweli Mchungu: Wengi Wenu Hamna Shida ya Pesa, Mna Shida ya Akili

Hebu tuwe wakweli kidogo.

Watu wengi hawana shida ya kukosa fursa.
Wana shida ya kukosa mtazamo.

Unasema huna hela,
lakini kila siku una bundle.
Una simu kali.
Una data.
Una muda wa kuscroll saa mbili.

Lakini bado unasema: “Hapa bongo maisha magumu.”

Maisha sio magumu.
Wewe umezoea kuyachezea.

Wengine wanatumia simu ile ile:

  • Kujenga biashara

  • Kujenga jina

  • Kujenga kipato

Wewe unaitumia:

  • Kuangalia story za watu

  • Kucheka video

  • Kulalamika comments

  • Kusema “nchi hii hamna kazi”

Unataka mafanikio,
lakini hutaki kubadilika.

Unataka pesa,
lakini hutaki kuwajibika.

Unataka kutoka,
lakini hutaki kuanza.

Kila mtu unayemuona juu leo:

  • Aliwahi kuwa sifuri

  • Aliwahi kuchekwa

  • Aliwahi kukosa

  • Aliwahi kuogopa

Tofauti ni moja tu:
Hakuamua kukaa chini.

Watu wengi wanapenda kusema:

“Bro, maisha ni magumu.”

Lakini hawapendi kusema:

“Bro, sijajipa presha ya kubadilika.”

Hakuna mtu atakayekuja kukuokoa.
Hakuna serikali itakayekupa ndoto.
Hakuna rafiki atakayekujenga maisha.

Kama hutachukua jukumu la maisha yako,
utakua expert wa kulalamika.

Na dunia haimlipi anayelalamika.
Inamlipa anayejisimamia.

Ukweli ni huu:

Ama utajenga maisha yako,
au utatumika kwenye maisha ya watu wengine.

Chagua mapema.

👉 Kama uko tayari kuacha kuwa mtazamaji na kuanza kuwa mchezaji, pata kitabu kupitia link hii: Siri 69 za Kupata Pesa

Usiseme “siku moja.”
Anza leo.
Maisha hayamsubiri anayesita.

0 comments

Leave a comment