Hebu tujiulize kwa uaminifu.
Je, kweli tatizo lako ni kukosa nafasi?
Au ni kukosa mwelekeo?
Unasema huna mtaji,
lakini una smartphone.
Una intaneti.
Una saa za TikTok.
Una muda wa kufuatilia maisha ya watu wengine.
Halafu unasema,
“Maisha hapa nyumbani ni magumu sana.”
Maisha hayajakukataa.
Ni wewe uliyeacha kuyachukua kwa uzito.
Wengine wanatumia zana hizo hizo ulizonazo:
-
Kujifunza
-
Kujenga skill
-
Kujenga brand
-
Kujenga kipato
Wewe unazitumia:
-
Kushangaa maisha ya watu
-
Kucheka memes
-
Kujibu comments
-
Kulalamika “hamna connection”
Unataka matokeo,
lakini hutaki mchakato.
Unataka mafanikio,
lakini hutaki maumivu ya kukua.
Unataka kutoka chini,
lakini hutaki kuanza pale ulipo.
Kila mtu unayemuona leo anaishi maisha unayoyatamani:
Aliwahi kukwama
Aliwahi kuchanganyikiwa
Aliwahi kukataliwa
Aliwahi kujiuliza, “Nitaweza kweli?”
Tofauti si kipaji.
Tofauti si bahati.
Tofauti ni uamuzi.
Wao waliamua kuendelea hata walipoogopa.
Watu wengi hupenda kusema:
“Maisha yamenikalia vibaya.”
Lakini hawapendi kukiri:
“Sijachukua jukumu la maisha yangu.”
Hakuna mtu atakayekuja kukuchukua mkono.
Hakuna mazingira yatakayokuwa perfect.
Hakuna siku maalum itakayokufanya uanze.
Ukipendelea kulaumu,
utakuwa bingwa wa sababu.
Na dunia haithamini sababu.
Inathamini hatua.
Ukweli mchungu ni huu:
Ama utajenga ndoto yako,
au utatumika kujenga ndoto za watu wengine.
Hakuna njia ya kati.
👉 Kama umechoka kuwa mtazamaji na uko tayari kuwa mhusika mkuu wa maisha yako, anza hapa: Siri 69 za Kupata Pesa kupitia link hii.
Usisubiri “wakati mzuri.”
Wakati mzuri ni sasa.
Maisha hayamsubiri anayehofia kuanza.
0 comments